Shirikisho la soka barani Afrika CAF limetuma barua ya ufafanuzi kuhusu adhabu ya Mtibwa Sugar.

Katika barua ya CAF kwenda kwa Katibu Mkuu wa TFF Kidao Wilfred,imesema Mtibwa Sugar wanaruhusiwa kushiriki katika mashindano y Kombe la Shirikisho lakini ikiwataka kuwasilisha nyaraka zinazothibitisha kulipwa kwa faini ya Dola 1500 pamoja na fidia kwa timu ya Santos ya Africa Kusini.

Mtibwa Sugar ilifungiwa kushiriki mashindano ya kimataifa April 2004 wakifungiwa miaka 3 na faini ya dola 1500.

TFF inafanya juhudi kubwa kuhakikisha jambo hilo linamalizika kabla ya Julai 20,2018 tarehe ya mwisho iliyotolewa na CAF nyaraka hizo kuwa zimewasilishwa.

Mtibwa Sugar ndio mabingwa wa Azam Sports Federation Cup na wataiwakilisha Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Africa.

Rais wa TFF Wallace Karia atuma salamu za pole msiba wa Profesa Majimarefu na mchezaji polisi Dar
Willian awapagawisha FC Barcelona, Paulinho afanywa chambo