Klabu ya Mtibwa Sugar imetoa taarifa ya kutumia Uwanja wa Manungu Complex kwenye mchezo ujao dhidi ya Simba SC, utakaochezwa Jumamosi (Januari 22).

Taarifa hiyo imetolewa na klabu hiyo ya Mkoni Morogoro kupitia Ukurasa wa Mtandao wa Kijamii wa Instagram wa Mtibwa Sugar.

Taarifa hiyo imeeleza: “Mchezo wetu unaofuata wa ligi kuu ya NBC dhidi ya @simbasctanzania utachezwa uwanja wa nyumbani MANUNGU COMPLEX jumamosi ya tarehe 22 saa 10:00 jioni.”

Timu hizo zitakutana kwa mara ya kwanza katika Uwanja wa Manungo Complex, kufuatia miaka yote Mtibwa Sugar imekua ikitumia Uwanja wa Jamhuri inapokutana na timu za Simba na Young Africans.

Tanzania kusikika tena Kimataifa
Msomi wa chuo kikuu alizwa na mwanamke wa 'Instagram'