Uongozi wa Klabu ya Mtibwa Sugar umesisitiza kufanya kila linalowezekana ili kufanikisha mapendekezo yatakayowasilishwa na Kocha Mkuu Salum Shaban Mayanga, ili timu yao ifanye vizuri kwenye Mzunguuko wa Pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mtibwa Sugar imemaliza Mzunguuko wa Kwanza ikishika nafasi ya Sita katika Msimamo baada ya kujikusanyia alama 22 zilizotokana na kushinda michezo Sita, ikitoa sare Minne na kuambulia sare mara Tano.

Afisa Habari wa Klabu hiyo yenye Mskani yake Makuu Manungu, Tuariani Mkoani Morogoro Thobias Kifaru amesema, Uongozi umedhamiria kuongeza nguvu kwa kufanya usajili wa Mchezaji yoyete atakayependekezwa na Kocha Mkuu, ima awe wa nje ama ndani ya Tanzania.

Amesema bado wanaamini kikosi chao kina nafasi ya kumaliza katika nafasi nne za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu, hivyo Uongozi umeweka nguvu kubwa kwa kumuamini Kocha Mayanga, ambaye wakati wowote atawasilisha ripoti ya Mzunguuko wa Kwanza uliofikia tamati jana baada ya mchezo wa Namungo FC dhidi ya Young Africans kupigwa Uwanja wa Majaliwa Mjini Ruangwa Mkoani Lindi.

“Tumedhamiria kufanya makubwa sana msimu huu, tumemaliza Mzunguuko wa Kwanza tukivuna alama 22, si haba kwa sababu hatua tulioipiga ni kubwa tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita, kwa kuhakikisha tunaendeleza mazuri, Uongozi unasubiri Ripoti ya Kocha Mayanga ili waifanyie kazi kwa vitendo.”

“Nikuhakikishie Mchezaji yoyote atayependekezwa na Kocha Mkuu Mayanga atasajiliwa Mtibwa Sugar kupitia Dirisha Dogo, Mtibwa Tumejipanga kupambana kweli kweli msimu huu, kwa sababu tunataka kumaliza nafasi nne za juu ili tukaiwakilishe nchi msimu ujao.” amesema Kifaru

Mtibwa Sugar itaanza Mzunguuko wa Pili wa Ligi Kuu kwa kuikabili Namungo FC katika Uwanja wa Manungu Complex Mkoani Morogoro, Desemba 16.

Geita Gold FC: Hatutasajili kwa Mihemko
Ihefu FC yadhamiria Mzunguuko wa Pili