Wachezaji sita wanaoitumikia klabu ya Mtibwa Sugar wameitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana (Ngorongoro Heroes) kwa ajili kusaka tiketi ya kufuzu AFCON 2019 chini ya umri wa miaka 20.

wachezaji hao ni kipa wa timu ya vijana ya Mtibwa Sugar Abuutwalib Msheli, Kibwana Ally Shomary (beki wa pembeni), Dickson Mwakasisili Job (beki ya kati) na Riphat Khamis Msuya (mshambuliaji).

Wachezaji wengine wawili ni Nickson Clement Kibabage (beki) anayetumikia kikosi cha Njombe Mji kwa mkopo wa miezi 6 na Muhsin Makame Malima (kiungo mshambuliaji) anatumikia kikosi cha Njombe Mji kwa mkopo wa miezi 6.

Klabu ya Mtibwa Sugar imeendeleza utamaduni wake wa kukuza vipaji na kikosi kilichoitwa cha Ngorongoro Heroes  ni timu iliyo ongoza kwa kutoa wachezaji wengi katika kikosi cha Ngorongoro Heroes jumla ya wachezaji 6 wameitwa katika kikosi hicho.

Ngorogoro Heroes chini ya Kim Poulsen na Oscar Milambo wanatafuta nafasi ya kufuzu katika michuano ya AFCON itakayofanyika nchini Nigeria mwakani.

Ngorongoro Heroes wana kibarua Machi 30 dhidi ya DR Congo jijini Dar es laam na baadae Ngorongoro Heroes watasafiri hadi Kishasa Congo Aprili 22 kwa ajili ya mchezo wa marudio.

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Machi 7, 2018
Video: Musiba anatumika vibaya, siwezi kupuuza maneno yake- Yericko Nyerere