Wakata miwa kutoka Manungu, Tuariani mkoani Morogoro (Mtibwa Sugar) wamerekebisha makosa yaliyopelekea kupoteza mchezo wa mwanzoni mwa juma hili dhidi ya Simba, kwa kuitandika Ndanda FC bao moja kwa sifuri.

Mtibwa Sugar wamepata ushindi huo katika uwanja wao wa Manungu Complex, na kujiongezea alama tatu muhimu kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka Tanznaia bara msimu wa 2017/18.

Bao pekee la Mtibwa Sugar katika mchezo wa hii leo dhidi ya Ndanda FC, limefungwa na mshambuliaji Kelvin Kiduku Sabato katika dakika ya 22 kipindi cha kwanza.

Mtibwa sasa imefikisha jumla ya alama 33 kwenye msimamo wa ligi, huku ikicheza michezo 23 na ikiwa nafasi ya 6.

Kwa upande wa Ndanda FC wameendelea kusalia katika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi, kwa kujikusanyia alama 23, baada ya kushuka dimbani mara 24 msimu huu.

Simba waendelea kulisogelea taji la ubingwa 2017/18
EXCLUSIVE: Tazama One the Incredible akiichambua mistari ya wimbo wake wa "Adoado Mixer"

Comments

comments