Kuna namna ya maisha ambayo kwa namna moja ua nyingine inachagiza maisha ya binadamu kuwa marefu na yenye furaha au kuwa mafupi na yenye karaha, tafiti zinaonesha kuwa kuna namna ya maisha ambayo ukiyaishi lazima uatongeza siku zako kisayansi.

Hivyo inashuriwa ili uishi maisha marefu mtindo wa maisha yako unapaswa kuwa hivi.

Hakikisha unapata mlo kamili au mlo wenye afya kulingana na mahitaji ya mwili, ulaji wa vyakula vya wanga kama ugali, wali, mihogo, mara kwa mara, husababisha mtu kunenepa na kuzidi uzito hivyo jiepushe kula vyakula vya aina moja kila siku, aidha hakikisha unajitahidi kupata chakula aina tofauti tofauti ili kujenga mwili na kuongeza siku za kuishi kwani kwa kufanya hivyo inasaidia kujiepeusha na magonjwa yasiyoambukiza kama kansa na magonjwa ya moyo.

Inashauriwa kufanya mazoezi, kwa ukawaida binadamu anatakiwa kufanya mazoezi angalau dakika 30 kila siku hii husaidia kuimarisha mwili.

Kunywa pombe kiistaarabu, inashauriwa kipimo cha mwanaume kunywa pombe kisizidi bia tatu au glasi ya 75ml ya mvinyo na kwa mwanamke zisizidi bia mbili au glasi ya mvinyo yenye 25ml.

Inashauriwa usivute sigara kabisa au bangi au kutumia bidhaa zitokanazo na tumbaku kwani bidhaa za tumbaku zina kemikali za sumu zinazoua seli za mwili na kuongeza hatari ya kupata maradhi ya moyo, saratani, kansa, na magonjwa ya njia ya hewa.

Matendo yasiyokufaidisha wewe mwenyewe au wengine ni sawa na kupoteza nguvu na muda, hivyo basi usipoteze muda kwa mambo yanayokutenga na upendo wa Mungu.

Hatma mgomo wa wahadhiri kujadiliwa leo
Tanesco yatangaza umeme kukatika Dar

Comments

comments