Aliyekuwa kocha msaidizi wa klabu ya Simba SC Selemani Matola, leo amesaini mkataba wa mwaka mmoja na timu ya Geita Gold FC inayoshiriki ligi daraja la kwanza Tanzania bara.

Novemba 11 mwaka huu, Matola aliandika barua kwa ajili ya kuomba kujiuzulu ndani ya Simba kwa madai kuwa hana maelewano mazuri na kocha mkuu Dylan Kerr.

Matola amekuwa kocha msaidizi kwenye kikosi cha Simba kwa muda mrefu baada ya kuitumikia Simba kama mchezaji na nahodha pia.

Geita Gold FC ipo kundi C na inafanya vizuri kwenye kundi hilo ikiwa inachuana kwa karibu na JKT Olijoro inayoongoza kundi hilo ikiwa na kileleni kwa pointi 14.

Kwenye kundi C kuna timu za Geita Gold FC, JKT Oljoro, Polisi Tabora, Panone FC, Mbao FC, Rhino Rangers, Polisi Mara na JKT Kanembwa.

Baada ya kutua kwenye kikosi hicho Matola atakuwa na kazi ya kuhakikisha anakisaidia kupanda daraja kwa ajili ya kushiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.

Dani Alves Amchongea Cristiano Ronaldo
Putin asema tukio la ndege ya Urusi kuangushwa na Uturuki ni sawa na ‘Kuchomwa kisu mgongoni’