Mtoto mwenye umri wa miaka 9 Khalid Hamisi, anayesemekana ni mgonjwa wa akili amefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye kisima cha mtu binafsi chenye urefu wa futi nane mtaa wa Bondeni, Wilayani Kaliua mkoani Tabora.

Akizungumza na Dar24Media Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Safia Jongo amesema kuwa mtoto huyo alikuwa anatoka kuchuma ubuyu na wenzake na ndipo tukio hilo likatokea

Amesema kuwa walipata tarifa kutoka kwa moja wa mtoto waliokuwa wameongozana na marehemu, mwenye umri wa miaka mitatu na nusu na ndipo timu ya uokoaji ilifika katika eneo la tukio na kukuta Khalid amefariki.

Aidha muhusika wa Kisima hicho yuko mikononi mwa Polisi kwa mahojiano zaidi, huku Kamanda Jongo akisistiza sheria kuchukua mkondo wake kwenye matukio ya uzembe kama hayo.

Kamanda Jongo amekili Mkoa wa Tabora matukio kama hayo ni mengi katika maeneo mbalimbali mkoani hapo kutokana na watu kuacha visima wazi lakini pia kutokufukia mashimo na mvua inaponyesha watoto hutumbukia na kupoteza maisha.

Jeshi la Polisi mkoani hapo kwa kushirikiana na Maafisa Afya kwa kufanya ukaguzi wa visima vilivyo wazi lakini pia kutoa elimu ya kwa wananchi ili kuhakikisha kutokujirudia kwa makosa kama hilo.

PICHA: Young Africans yawasili kinyonge Dar
Mukoko Tonombe aomba radhi Young Africans