Kenya, mtoto mmoja ambaye ni mwanafunzi mwenye umri wa miaka 11 ameamua kujiua kwa kujinyonga baada ya ombi lake la kuhamishwa shule kukataliwa.

Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Ongata Rongai ambapo mtoto huyo ameamua kuchukua uamuzi huo mgumu baada ya mama yake kumuambia hana uwezo wa kumpeleka shule binafsi anayotaka, na kumtoa kwenye shule ya umma aliyokuwa akisoma.

Baada ya mama yake kutoka kwenda dukani mtoto huyo ambaye ni wa kwanza kuzaliwa kwenye familia ya watoto watatu, alichukua kamba na kujinynga sebuleni kwao, na mama mtu kukuta mwili wa mtoto wake ukining’inia.

Kwa mujibu wa mama wa mtoto huyo hakukuwa na ugomvi wowote baina yao zaidi ya kushindwa kutekeleza ombi lake.

Hivyo jeshi la polisi limesema linafanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo, kwani wanashindwa kuelewa kwa nini mtoto huyo hakwenda shule na kuamua kubaki nyumbani,  wakati shule zimeshafunguliwa.

 

 

Afungua kesi mahakamani akitaka ukeketaji uhalalishwe
Majaliwa agawa kadi za matibabu kwa wazee 280

Comments

comments