Mtoto  shukuru kisonga aliyekuwa na tatizo la kunywa mafuta na kubwia sukari leo ameachana na matumizi ya vitu hivyo mara baada ya kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili hivyo kuanza kunywa uji na soda.

Hayo yamesemwa na mama mzazi wa mtoto huyo, Mwanahabibi Mtenje wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam, amesema kuwa amepata faraja kubwa kuona mwanae anaachana na utumiaji wa mafuta, maziwa na sukari kwani alikuwa katika hali isiyokuwa ya kawaida.

“Kwakweli ni jambo la kumshukuru mungu kwani hali ya mwanangu haikuwa ya kawaida, lakini kwa sasa ameanza kutumia uji na soda kitu ambacho mwanzoni kilikuwa ni kigumu sana”, amesema Mwanahabibi huku akibubujikwa na machozi.

Hata hivyo katika mkutano huo na waandishi wa habari, Mwanahabibi alikuwa ameambatana na Daktari bingwa wa magonjwa ya Damu, Dkt. Stella Rwezaura ambaye ametoa majibu ya mtoto huyo baada ya kumpatia matibabu.

Aliyekuwa Rais wa Korea Kusini Afikishwa Mahakamani, Pingu Mikononi
Basata Wamsaka Ben Pol kuhusu picha alizopiga akiwa ‘mtupu’