Dar es Salaam jana kupitia vyombo mbalimbali vya habari iliripotiwa juu ya taarifa za kupotea kwa mtoto mwenye umri wa miaka 3 aliyefahamika kwa jina la Beauty Yohana ambaye alichukuliwa na mtu asiyejulikana akidai kuwa ni dada yake wa kazi.

Mtoto huyo amepatikana leo Jumanne ya Septemba 25, maeneo ya Kitunda katika kituo cha Polisi akiwa mzima wa afya.

Yohana Isango ambaye ni baba wa mtoto huyo amesema wakati ibada ikiendelea Kanisa la FPCT lililopo Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam alionekana binti mmoja mweusi akiwa nje ya kanisa na baadaye alikwenda chumba cha watoto na kumtaka Beauty ili akanywe dawa.

Mtoto Beuty alikuwa kanisani kwenye mafundisho ya ‘Sunday school’ ndipo dada huyo aliyejifanya dada wa kazi kumuomba toka kwa mwalimu wake ili amchukue akampe dawa na kukimbia naye kusikojulikana.

Aidha, Mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Facebook, Instagram ilitumika kutangaza juu ya kupotea kwa mtoto huyo, hatimaye leo mtoto huyo amepatikana akiwa mwenye afya njema na salama.

Taarifa juu ya kukamatwa kwa dada huyo aliyehusika na utekaji wa mtoto Beauty bado hazijawekwa wazi, endelea kufuatilia Dar24 tutakujuza zaidi

 

Video: Cardi B ajibu tetesi za Rihanna kumpiga chini Instagram
Utafiti: Upweke kuwaumiza mamilioni zaidi