Mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 11 ameripotiwa kumuua mdogo wake wa kike mwenye umri wa miaka miwili kwa risasi na baadaye kujipiga risasi pia, nchini Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na jeshi la polisi, mtoto huyo alikuwa anachezea bunduki ya baba yake ambayo ilikuwa imesajiliwa kisheria alifyatua risasi kwa bahati mbaya ambayo ilichukua uhai wa mdogo wake.

Baada ya kuona amemuua mdogo wake, mtoto huyo alijigeuzia bunduki na kujifyatulia risasi pia.

Taarifa hiyo ya jeshi imeeleza kuwa tukio hilo limetokea Februari 3 mwaka huu katika eneo la KwaZulu-Natal majira ya saa tano na dakika 50 usiku.

Baada ya kujipiga risasi, mtoto huyo alikimbizwa katika hospitali iliyopo karibu lakini alipoteza maisha wakati anapatiwa matibabu.

“Watu wanaomiliki silaha za moto wanatakiwa kuzingatia sheria ya umiliki silaha na kuchukua tahadhari kwani kwenda kinyume na sheria hiyo kunaweza kusababisha vifo visivyo vya lazima,” imeeleza taarifa ya Jeshi hilo.

Hassan Dalali atupa dongo Jangwani
Aliyehusika mauaji ya Radio atiwa mbaroni

Comments

comments