Neema ya Mungu imemshukia mtoto mchanga mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu aliyekuwa miongoni mwa wahanga waliofunikwa na jengo la ghorofa sita liloloporomoka Ijumaa iliyopita katika mtaa wa Huruma, jijini Nairobi nchini Kenya.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation la Kenya, mtoto huyo ameokolewa akiwa hai majira ya saa kumi usiku na kukimbizwa hospitalini. Kamanda wa kitengo cha taifa cha kudhibiti majanga nchini humo, Pius Maasai anasema hali ya mtoto huyo inaendelea vizuri.

Serikali ya Kenya imeeleza kuwa watu 22 wamethibitika kupoteza maisha kutokana na ajali hiyo huku wengine takribani 90 hawajapatikana. Imeelezwa kuwa tayari watu 136 wameokolewa kutoka kwenye jengo hilo hadi kufikia leo.

Jeshi la Polisi nchini humo limeeleza kuwa jengo hilo halikufaa kwa makazi na kwamba wamiliki wa jengo hilo wanashikiliwa na jeshi hilo na watafikishwa mahakamani mapema leo.

 

Mambo 10 Ya Ajabu Yaliyoizidi Kete Leicester City Kushinda EPL
Nani Kutangulia Fainali Ya Ligi Ya Mabingwa Barani Ulaya Leo?