Mtoto wa kike wa Chris Brown, Royalty amefuata nyayo za baba yake akiwa na umri mdogo ambapo leo anatarajiwa kuzindua biashara ya mavazi yake (clothing line).

Kwa mujibu wa TMZ, Royalty atafanya biashara hiyo kwa kujikita katika nguo za watoto kwa lengo la kuwafikia mashabiki wake wenye umri mdogo..

Mama yake Royalty, Nia Guzman anaripotiwa kufanya kazi kubwa katika kuitangaza na kuiandaa biashara hiyo ya mwanae.

Kwa mujibu wa ‘post’ aliyoweka, Nia Guzman kwenye mtandao wa Instagram nguo hizo zitaingia sokoni rasmi leo huku akiwataka wateja na mashabiki kujiunga na orodha ya barua pepe kupitia mtandao wa RoyaltyBrown.com.

Hata hivyo, haijaelezwa wazi kama Chris Brown pia ana mkono wake kwenye biashara hiyo inayoungwa mkono hasa na mama mtoto wake huyo ambaye walikuwa kwenye mgogoro mzito hapo awali.

Wakati Royalty anaingiza mzigo huo sokoni, baba yake anaendelea kupigia debe mavazi yake mapya aliyoyabatiza jina la ‘Black Pyramid’.

Tabora yajipanga kuzitumia fursa Bomba la mafuta
Wakenya wazidi kumiminika Tanzania, wahofia machafuko