Mtoto wa kwanza wa kiume wa kiongozi wa Cuba, Fidel Castro ameripotiwa kujiua katika eneo la Havana, kwa mujibu wa kituo cha habari cha taifa hilo.

Fidel Ángel Castro Díaz-Balart aliyekuwa na umri wa miaka 68, alikutwa amejiua Alhamisi wiki hii na taarifa zinaeleza kuwa alikuwa akisumbuliwa na msongo wa mawazo kwa muda mrefu.

“Fidel Castro Díaz-Balart aliyekuwa akitibiwa na kundi la madaktari kwa miezi kadhaa kutokana na kusumbuliwa na msongo wa mawazo, amejiua asubuhi hii,” limeripoti gazeti la Granma.

Mtoto huyo wa Fidel Castro alipewa jina la utani la Fidelito (Fidel Mdogo) kutokana na namna alivyokuwa akifanana na baba yake.

Wakati wa enzi za uhai wa baba yake akiwa kiongozi, mtoto huyo alipatiwa mafunzo ya nyuklia na umoja wa Kisovieti.

Amejiua ikiwa ni mwaka mmoja baada ya baba yake kufariki dunia akiacha wosia mzito kuhusu nchi hiyo hasa na uhusiano wao nan chi za Magharibi.

Breaking News: Wahamiaji haramu 90, wahofia kufa maji
Marubani 2 wafariki dunia baada ya kulipukiwa na ndege