Wahenga hawataachwa kutajwa kwenye kizazi hiki kwa kuturahisishia maelezo… walisema ‘mtoto wa nyoka ni nyoka na maji hufuata mkondo’, ndicho kinachoonekana hivi sasa kwenye familia ya bwana na bibi Carter aka Jay Z.

Mtoto wa kike wa nguli huyo wa hip hop, Blue Ivy mwenye umri wa miaka mitano na nusu ameonekana kufuata nyayo za baba yake baada ya kusikika kwenye albam hiyo akirap kwa takribani sekunde 45 bila kuweka kituo kikubwa.

Kwenye michano hiyo iliyopewa jina la ‘Blue’s Freestyle/We Family”, anasikika akipita na mtindo wa kurap wa baba yake.

“Never seen a ceiling in my whole life…Boom shakalaka, boom shakalaka, everything in shaka, everything in faka,” anarap Blue Ivy.

Kwa tafrisi isiyo rasmi, Blue Ivy anajigamba kuwa hajawahi kuona kizuizi juu [anapopanda] kwenye maisha yake yote, na kila kitu kwake ni ‘mambo mswano’.

Jay Z alianza kumtabilia mwanae kuwa rapa, baada ya kumshirikisha kwenye wimbo wake wa ‘Glory’ mwaka 2012, akimuimbia kuwa yeye ni  kitu cha thamani zaidi alichowahi kuwa nacho kwenye maisha yake.

Video: Mwakyembe amtumbua Malinzi wa BMT
Airtel na GSMA waandaa mashindano ya suluhu za mfumo wa malipo ya pesa kupitia simu za mkononi