Blue Ivy, mtoto wa Jay  Z na Beyonce Jana aliwaacha watu mdomo wazi baada ya kuweka dau la $19,000 akishindania kununua mchoro kwenye mnada.

Mnada huo uliofanyika Jumamosi hii ukiratibiwa na mama yake Beyonce, Tina Knowles na mumewe Richard Lawson ulikuwa na lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya mahitaji maalum jijini Los Angeles nchini Marekani.

Blue Ivy aliweka mkono wake juu kwa mara ya kwanza na kutaja dau la $17,000 kwa ajili ya mchoro wa mtoto Sidney Poitier lakini alipoona kuna mtu ‘amepanda dau’ aliongeza hadi $19,000.

Kipande cha video kinachosambaa mtandaoni kilimuonesha Jay Z akifanya utani kumkataza asinyooshe mkono tena kuongeza dau baada ya mara ya kwanza, lakini Blue Ivy alinyoosha mkono wake zaidi.

Hata hivyo, Tyler Perry ndiye aliyeshinda kwa kuweka dau la $20,000 lililokosa mpinzani.

Mayweather athibitisha kushiriki pambano la ngumi na mateke
Taesa yatoa ufafanuzi jinsi ya kujisajili ajira 10,000 bomba la mafuta Hoima