Binti wa rapa maarufu wa nchini Marekani Lil Wayne aitwaye Reginae Carter amefunguka kwa mara ya kwanza akiitetea nafasi ya baba yake pamoja na urithi wa makubwa aliyoyafanya kwenye tasnia ya muziki nchini Marekani kutokana na kukithiri kwa kasumba ya baadhi ya watu kumlinganisha rapa huyo na wasanii wachanga wanaofanya vizuri kwa sasa nchini humo.

Siku ya Jumanne (Januari 3), mtandao wa kustream muziki online uitwao MyMixtapes ulichapisha swali kwenye ukurasa wake wa twiter likiuliza “Nani anaenda kwa bidii zaidi kati ya Lil Wayne au Lil Baby wa Sasa?” Tweet iliyofanikiwa kutazamwa zaidi ya mara 700,000 hadi kufikia Jumamosi ya (Januari 7), na ilikuwa imechapishwa (retweets) karibu mara 1,000.

Lil wayne kwenye picha ya pamoja na binti yake Regina. Photo: Getty / Getty

Swali hilo liliibua majadala mzito kwenye mitandao mbali mbali ya kijamii huku kila mmoja akizungumza la kwake zaidi rapa Lil wayne akishabihishwa na wasanii wapya kwenye tasnia, jambo ambalo baadhi ya mashabiki wa nyota huyo wamekuwa wakilipinga vikali.

Ikiwamo mtoto wake Regina Carter, ambaye siku ya Ijumaa (Januari 6), aliamua kuvunja ukimya ili kuitetea naafas ya baba yake kwenye tasnia ya muziki nchini Marekani, ambapo alidhihirisha kupinga vikali ushindanishwaji huo bila kusema chochote kibaya kuhusu rapa Lil baby ambaye ametajwa kushindanishwa na Wayne.

“Litoeni jina la baba yangu midomoni mwemu, Nadhani wote mnahaja ya kuacha kumlinganisha baba yangu na hawa watoto wapya kwenye muziki, Kila mtu ana talanta ya hali ya juu na ni mzuri, Waacheni wafanye kile wanachoweza ila muda utasema, lakini muondosheni baba yangu kwenye ushindani huo” ameandika Regina.

Pamoja na maoni ya mashabiki juu ya rapa Lil wayne, yapo mengi makubwa ambayo yanamuweka nyota huyo kwenye kundi la miongoni mwa wasanii waliofanya makubwa sana kwenye tasnia ya muziki Duniani.

Weezy mpaka sasa anajumla ya Albamu 14 alizoachia kati ya mwaka 1999 na 2020, sita kati hizo zimepata vyeti vya paltnumz (multi-platinum certifications) zitolewazo na Record Industry Association of America (RIAA) na album nyingine tatu zilichumpa mpaka kwenye hadhi ya Platnum.

Wakati huo huo, Wayne pia ametoa jumla ya EP zisizopungua tano pamoja na mixtapes 29, huku akishirikiana na nyota wengine kama Drake, JAY-Z, Kanye West, DJ Khaled, Fall Out Boy, Weezer, Destiny’s Child, Chris Brown na Shakira, ikiwa ni pamoja na kuhusika kwake na kunyanyua vipaji vya wasanii wenzake aliokuwa nao chini ya Cash Money na baadhi waliosainiwa chini ya Young Money.

Kwa makubwa aliyoyafanya, taswira ya kipekee ya rapa Lil Wayne, kiasi na ubora wa pato lake umemfanya mzaliwa huyo wa New Orleans kutajwa kwenye orodha nyingi za wasanii bora wa Hip Hop kwa miaka mingi.

Lil Wayne baada ya kupokea tuzo ya BET 2028. photo: Bilboard News

Mpaka sasa, kwa kipindi chote ambacho amekuwa kwenye tasnia ya muziki, Wayne amefanikiwa kupata jumla ya tuzo 143, zikiwemo tuzo nne za Grammy, Tuzo nne za Billboard na Tuzo nane za BMI, huku Mtunzi Bora wa Mwaka wa Urban akiibuka kinara kwa vipindi viwili mfululizo yaani mwaka 2009 na 2010.

Ingawa wengine wanaweza kusema kuwa sio haki kutathmini mafanikio ya Lil Baby kwa kumlinganisha Weezy F. lakini nyota huyo anaonekana kuwa njiani akizifuata nyayo za Wayne, hii ni kutokana na makubwa ambayo Lil baby ameonekana kuyafanya tangu alipoingia rasmi kwenye tasnia ya muziki hasa umahiri na mengi makubwa aliyofanya hasa ndani mwaka 2022.

Mnamo Oktoba, nyota huyo mzaliwa Atlanta huko nchini Marekani alikua msanii mchanga zaidi kuwahi kuingiza nyimbo 25 kwenye chati za Billboard Hot 100 kwa wakati mmoja, na nyimbo zote 23 kutoka kwenye albamu yake mpya ya ‘It’s Only Me’ zikifanikiwa kuingia kwenye chati mbali mbali katika wiki ya kwanza tu, tangu album hiyo kutolewa.

Also read: ‘Kama muziki haujawahi kukulipa achana nao’ – Sallam SK

Bei mpya ya vifurushi kutangazwa
'Kama muziki haujawahi kukulipa achana nao' - Sallam SK