Imeelezwa kuwa mtoto wa Malkia Elizabeth II wa Uingereza, mwanamfalme Charles mwenye umri wa miaka 71, amekutwa na maambukizi ya virusi vya Corona baada ya kufanyiwa vipimo.

Msemaji wa familia hiyo amesema Charles aliamua kupima baada ya kuanza kujisikia vibaya lakini kwa sasa anaendelea vizuri.

Mkewe The Duchess of Cornwall, mwenye umri umri wa miaka 72 pia amefanyiwa vipimo , lakini vimeonyesha kuwa hana virusi hivyo.

Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni za wizara ya afya na huduma za jamii, kwa sasa kuna visa zaidi ya 8,000 vilivyothibitishwa vya coronavirus nchini Uingereza ingawa idadi kamili ya visa huendaikawa ni ya juu zaidi . Badhi ya wagonjwa 422 tayari wamefariki.

Mara ya mwisho mwanamfalme alionekana katika shughuli za umma tarehe 12 Machi lakini amekua akifanyia kazi zake nyumbani kwa wiki chache zilizopita abako aliendesha mikutano ya kibinafsi na watu waliokutana nae wamefahamishwa kuhusu maambukizi aliyoyapata.

Miquissone apandisha bendera Msumbiji
Serikali yapokea msaada wa Bilionea Jack Ma, vifaa vya kukinga Corona

Comments

comments