Uganda, Polisi wilayani Bududa mashariki  wanamsaka mwanafunzi wa miaka 10 katika shule ya msingi Buwali aliyetoroka na baba yake mara baada ya kumchoma kisu na kumuua mwenzake kwa kisa kilichodaiwa kuwa aliporwa mpenzi wake.

Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Bududa (DPC) Bwana Jaffar Magayisi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la mauaji na wamesema kuwa kijana huyo aliyeuawa ana miaka 16  na anafahamika kwa jina la Sam Watsosi.

Tukio hilo limetokea siku ya Jumapili ambapo baada ya kutokea kwa tukio hilo Watsosi alikimbizwa hospitali ya Bududa akiwa anavuja damu nyingi hali iliyopelekea kupoteza maisha siku ya jumatatu jioni.

Kuna mvutano mkubwa katika eneo hilo kwani ndugu za marehemu walitishia kushambulia familia ya mtuhumiwa kwa kulipiza kisasi.

Lakini DPC aliwataka familia ya Watsosi itulie, akisema mtuhumiwa atakamatwa na kushtakiwa kwa mauaji mahakamani.

Bwana Charles Mutabali Kibeti, mwenyekiti wa LCIII alisema “Inashangaza sana kuwa mtoto wa miaka 10 anaweza kuwa na rafiki wa kike, ambaye yuko tayari kufanya chochote kumlinda akiwa na umri mdogo,”

 

Maporomoko ya theluji yaua 160
Padri aliyefungisha ndoa ya Stamina afunguka

Comments

comments