Jijini Dar es salaam, Binti wa miaka 20 amemuua mdogo wake wa miaka miwili kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali kitovuni kisha kumficha uvunguni mwa kitanda nyumbani kwao kigamboni.

Emmanuel Lukula ambaye ni kamanda wa polisi Mkoa wa Temeke leo hii tarehe 25, Aprili amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

” Ni kweli tukio hilo limetokea juzi, aliyefanya hilo tukio ni binti wa miaka 20 ambaye ni ndugu wa mama wa marehemu. Si mfanyakazi wa ndani kama wengine wanavyodai alimchoma huyo mtoto na kumlaza kifudifudi uvunguni kisha akaondoka kuelekea kwa mwanaume anayedaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi,” amesema Kamanda Lukula.

Binti huyo kwa sasa anashikiliwa na polisi kwa kufanya tukio hilo la kinyama na alipokamatwa alikwenda kuwaonyesha uvungu wa kitanda alikomficha mdogo ake.

 

Nikki wa pili: Unyonge wa nini?
TLS waonywa, watakiwa kuacha uanaharakati

Comments

comments