Paris Jackson ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mfalme wa Pop duniani, Michael Jackson amejitokeza kumkingia kifua baba yake kufuatia sakata la ripoti zilizovuja zikionesha kuwa polisi walinasa picha za watoto wakiwa uchi na nusu uchi kwenye himaya ya baba yake.

Paris ametumia mdandao wa tweeter kupinga vikali madai yaliyoripotiwa na media kuhusu tukio hilo akiwataka watu kuachana na tuhuma hizo alizoziita ‘takataka’ zinazotaka kumchafua baba yake.

“Bahati mbaya, mambo hasi yatauza siku zote, ‘nawaomba wote kuzipotezea hizo takataka na wadudu wanaojitengenezea kazi wakitaka kumchafua baba yangu,” aliandika Paris na kuambatanisha picha inayomonesha Michael akilamba kidole cha ‘kati’.

Tweet ya Mtoto wa Michael

Mwanzoni mwa wiki hii, Radar Online ilitoa ripoti ya polisi inayoaminika kuwa imetoka kwa Mkuu wa Polisi wa Santa Barbara zikiwa na picha nyingi na maelezo kuhusu Michael Jackson, picha hizo zinaaminika kuwa za porno za watoto zilizopatikana kwenye jumba lake, ikiwa ni miaka saba baada ya kifo chake.

Serikali Yaombwa Kufanya Marekebisho ya Sheria ya Mirathi
Mbunge Wa CCM Amvaa Wa Chadema, Adai 'Ametamani Mwanaume Wa Mtu Mwingine’