Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na maafisa wa ujasusi wa Marekani, imeeleza kuwa mtoto wa kiume wa aliyekuwa muasisi wa al – Qaeda, Osama Bin Laden, Hamza Bin Laden ameuawa katika shambulio, huku bado haijawekwa wazi juu ya tarehe na mahali shambulio lilipo fanyika.

Hapo awali baada ya Hamza kutoa jumbe mbalimbali za sauti na video akitoa wito wa kufanya mashambulio dhidi ya Marekani na nchi nyingie, Mwezi Februari, Serikali ya Mrekani aliahidi kutoa dola milioni moja kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kutambua mahali alipo.

Kwa mujibu wa mashirika ya habari ya NBC na New York Times, Hamza Bin Laden aliyekisiliwa kuwa na umri wa miaka 30, aliwatolea wito wapiganaji wa jihadi kulipiza kisasi juu ya mauaji ya baba yake aliyeuawa na kikosi cha Marekani nchini Pakistan mwaka 2011.

Kijana huyo aliaminika kuwa katika kifungo cha nyumbani nchini Iran, lakini ripoti nyingine zilieeleza kuwa huenda alikuwa akiishi katika mataifa ya Afhanistan, Pakistan na Syria kwani Saudi Arabia ilimnyang’anya uraia mwezi Machi.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilisema kuwa nyaraka zilizokamatwa katika uvamizi kwenye nyumba ya Baba yake ya Abbottabad, Pakistan mwaka 2011, zinaonesha kuwa Hamza alikuwa anaandaliwa kuchukua utawala wa al-Qaeda.

Hamza, alimuoa Binti wa Abdullah Ahmed al-Masri, ambaye anatafutwa kwa madai ya kuhusika katika mashambulio ya ugaidi ya mwaka 1998 dhidi ya balozi za Tanzania na Kenya.

Kundi la al-Qaeda lilianzishwa na Osama Bin Laden, amabalo lilitangaza “vita vitakatifu” dhidi ya Wamarekani, wayahudi na washirika wo, lilitikisa ulimwengu hasa septemba 11, 2001 lilipo shambulia Marekani lakini katika kipindi cha miongo kadhaa sasa umaarufu wake umepungua baada ya kuibuka kundi la Islamic State.

 

Waziri Kamwelwe aomba jengo la Terminal II likarabatiwe
Tanzania, Zimbabwe zatiliana saini hati tano za makubaliano ya ushirikiano