Mwanamziki maarufu wa bongo fleva Nandy ameamua kumuajiri Mwachi mtoto wa marehemu Ruge Mutahaba kuwa DJ wake rasmi kuanzia tamasha ambalo ataanza nalo Sumbawanga siku ya EID.

Kauli hii imethibitishwa kupitia mtandao wa instagram baada ya Nandy kukoment officialnandy DJ na kuonekana kuwa nandy ameamua kumpatia Mwachi nafasi hiyo.

Hata hivyo watu wengi wamekuwa wakijiuliza maswali, uhusiano uliopo kati ya Nandy na mtoto wa kwanza wa marehemu Ruge, hivi karibuni mwanamuziki huyo aliweka wazi mahusiano yake ya kimapenzi yaliyokuwepo kati yake na Ruge kwenye mahojiano na Millard Ayo.

Hata hivyo mashabiki wamekuwa na kiu ya kujua kama kweli Nandy amempa shavu hilo Mwachi.

Kumbukizi: MV Bukoba na simulizi iliyoiliza Dunia
LIVE: Rais Magufuli akipokea gawio la Serikali kutoka TTCL

Comments

comments