Mtu aliyethibitika kuwa na umri mkubwa zaidi duniani amefariki akiwa na umri wa miaka 117, kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa leo.

Chiyo Miyako ambaye alikuwa raia wa Japan alifariki Jumapili iliyopita alipokuwa amelazwa hospitalini ingawa ugonjwa uliokuwa unamkabili haukuwekwa wazi.

Miyako alithibitishwa kuingia kwenye rekodi ya kitabu cha rekodi ya dunia cha Guinness, akitajwa kuwa mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani anayeishi na pia mwanamke mwenye umri mkubwa zaidi duniani anayeishi.

Kwa mujibu wa rekodi, Miyako alizaliwa Mei 2 mwaka 1901 katika mkoa wa Kansai, eneo la Wakayama nchini Japan.

Familia yake imemuelezea kama mwanamke aliyekuwa mcheshi na wa pekee wakati wa maisha yake. Wameeleza kuwa moja kati ya sifa yake kuu ilikuwa uvumilivu.

Wameeleza kuwa alikuwa anapenda kula vyakula vya Kijapan aina ya ‘shush na eel’.

Apumzike kwa Amani!

Korea Kaskazini yarejesha mabaki ya Wamarekani waliokufa vitani
Mkuu wa Majeshi Iran amvaa Trump, ‘anzisha tumalize’