Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro limesema kuwa mtuhumiwa hatari wa uhalifu ameuwawa na kukutwa na silaha aina ya SMG, risasi 24, simu 19 na laini 58, mara baada ya majibizano ya kurushiana risasi.

Hayo yamesemwa na kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Hamisi Issah ambapo amesema kuwa mtuhumiwa huyo aliuawa juzi saa tisa alfajiri wilayani Rombo na watu wanaodaiwa kuwa watuhumiwa wenzake.

Aidha, kwa mujibu wa taarifa hiyo, mtuhumiwa huyo pamoja na mkewe walikamatwa jijini Dar es Salaam na baada ya kuhojiwa na polisi anadaiwa kueleza matukio mbalimbali ya ujambazi aliyoshiriki.

“Polisi waliandamana naye chini ya ulinzi mkali hadi Moshi kwenye dampo lililopo karibu na kiwanda cha ngozi ambapo bunduki ilipatikana ikiwa imefukiwa ardhini ikiwa na risasi 24. “Muda wote alitoa ushirikiano mkubwa kwa polisi na alivyokuwa akisimulia matukio aliyoyafanya mwili unaweza kusisimka. Simu tatu kati ya 19 tumegundua ziliporwa hapa Moshi,” amesema Kamanda Issah.

Hata hivyo, ameongeza kuwa katika mahojiano hayo inadaiwa mtuhumiwa huyo aliwaeleza polisi juu ya mpango uliokuwapo wa kufanya tukio la ujambazi katika kijiji cha Chilio, kata ya Holili wilayani Rombo juzi alifajiri mkoani Kilimanjaro.

 

Trinidad na Tobago yaizima Marekani, ndoto za 2018 zayeyuka
Aguero arejea mazoezini baada ya kupata ajali