Kijana Issack Habakuki Emily, anayekabiliwa na kesi ya kutumia lugha chafu dhidi Rais John Magufuli kupitia ‘comment’ yake kwenye mada iliyowekwa kwenye mtandao wa kijamii amepewa dhamana.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha kutupilia mbali maombi ya upande wa mashtaka yaliyoitaka mahakama hiyo kutompa dhamana mtuhumiwa huyo. Upande huo wa mashtaka uliitaka Mahakama kutompa dhamana mtuhumiwa huyo kwa sababu ya usalama wake kwakuwa angeweza kudhuriwa na wananchi wenye hasira na pia angeweza kuingilia upelelezi unaoendelea.

Hakimu wa Mahakama hiyo, Augustine Rwezile alisema Mahakama hiyo imechukua uamuzi huo kwakuwa sababu za upande wa mashtaka hazitoshi kueleza namna ambavyo angeweza kuingilia upelelezi wa kesi hiyo au kudhurika.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Machi 17 mwaka huu alipokuwa akichangia katika mada kupitia akaunti ya mtandao wa kijamii wa kituo cha runinga cha Clouds, kinyume cha Sheria ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 17 mwaka huu itakaposikilizwa tena.

 

Rais Magufuli amteua Hamphrey Polepole Kuwa Mkuu wa Wilaya Musoma
Jerry Muro atuhumiwa kuwalaghai wachezaji wa Simba