Mshukiwa namba moja wa shambulio la kigaidi lililotokea jana nchini New zealand jijini Christchurch, na kuua watu 49, Brenton Terrant (28) amefikishwa tayari mahakamani kwa kuanza kusikiliza shitaka lake linalomkabili.

Waziri Mkuu wa nchi hiyo Jacinda Ardern amesema kuwa licha ya kosa la Mauaji ya kigaidi mshukiwa huyo amekutwa pia  na Bunduki tano pamoja na leseni tano za umiliki wa silaha za moto ambo ni kinyume na sheria za New Zealand.

Tarrent ataendelea kuwa chini ya ulinzi hadi April 5, ambapo atafikishwa Mahakamani tena, huku washukiwa wengine wawili bado wanaendelea kuhojiwa na polisi na hadi sasa hakuna hata mmoja mwenye historia ya uhalifu.

Alipozungumza na waandishi wa habari Waziri Ardern amesema kuwa silaha ambazo zimetumika katika shambulio hilo ni zakisasa zaidi na gari la mshukiwa limekutwa na silaha nyingi yakiwepo mabomu, jambo linaloashiria kuwa alikuwa na mpando wa kuendelea na mashambulio maeneo mengine tofauti.

Nakusisitiza juu ya umuhimu wa kuwarudisha marehemu kwa wapendwa wao haraka iwezekanavyo, na zoezi la kukusanya miili na kuitafuta bado linaendelea ndani na nje ya misikiti.

Aidha ametoa ahadi kuwa Serikali yake itatoa misaada ya kifedha kwa waathirika ambao wamepoteza ndugu waliokuwa wanategemewa katika familia kama wazazi na walezi.

Hili ni shambulio kubwa la kigaidi kuwahi kutokea New Zealand, ambapo watu 49 wamepoteza maisha , 48 wamejeruhiwa kati yao kuna watoto wawili, na miongoni mwa waliofariki wantokea nchi za Bangladesh, India na Indonesia.

Kula vyakula hivi kuokoa Nywele zako
Video: Lowassa ataishi vipi na CCM hii? Sababu halisi za kurudi hizi hapa (Makala)