Aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni (CUF), na kuhamia CCM, Maulid Mtulia ametii agizo la chama hicho lililomtaka kuripoti leo Jumanne ofisi ya CCM mkoa kwa ajili ya kuchukua maelekezo ya uchaguzi.

Hatua hiyo imekuja baada ya wiki iliyopita CCM kutangaza kuwarudisha kugombea majimbo yao waliokuwa wabunge Maulid Mtulia (Kinondoni-CUF) na Dk Godwin Molell (Siha-Chadema) ambao wamejiunga na chama hicho tawala.

Mtulia alitangaza kujiuzulu nafasi ya ubunge Desemba 2 mwaka jana huku akisema amefikia uamuzi huo bila kushawishiwa na mtu yeyote na amebaini Serikali ya CCM inafanya kazi kubwa ya kutekeleza ilani na imefanya vizuri katika mambo mengi ambayo upinzani iliahidi kuyatekeleza.

Wakati Dk Molell alijiuzulu Desemba 14 huku akieleza amefikia uamuzi huo akiwa na akili timamu na hakushinikizwa na mtu yeyote.

Lowassa amfuata Magufuli Ikulu
Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema atimkia CCM