Mtumbwi wa asili uliotengenezwa kutokana na taka za plastiki ambazo zimekusanywa kutotka katika fukwe za bahari ya hindi unatarajiwa kuanza safari yake mwezi ujao kutaka Lamu hadi Zanzibar.

Ujenzi wa mtumbwi huo ni kwa udhamini wa kampeni ya umoja wa mataifa (UN) katika kutokomeza  uchafuzi wa taka zinazotokana na plastiki katika Bahari.

Ikiwa na lengo la kushirikisha jamii inayoishi katika fukwe za bahari ya Hindi Afrika mashariki, katika kutokomeza utupaji taka za plastiki kwenye bahari kwa kuwaonesha njia mbadala za matumizi ya plastiki.

Mtumbwi huo umekuwa wakwanza waaina yake Duniani kutengenezwa kutokana na makopo na mifuko ya plastiki, ambao umetumia tani 10 za plastiki hadi kukamilika.

Moja ya washiriki wa mradi huo wa boti ya plastiki  Ben Morison, amesemakuwa walishawishiwa kutengeneza kitu kitakacho wavutia wananchi waishio pwani ya Kenya na Zanzibar kushiriki.

Katika nchi za Afrika uchafuzi wa bahari umekuwa tishio kwa kupoteza vyakula, kwani zaidi ya watu milioni 12 wanategemea uvuvi kupata chakula, hivyo uchafuzi wa bahari ni tishio kwa maisha yao.

kitendawili cha masoko ya mazao jamii ya kunde kuteguliwa
Mpinzani apinga matokeo ya Urais wa DRC Mahakamani