Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema kuwa mpaka kufikia Desemba 14, 2018 wakulima 130,163 wamelipwa jumla ya shilingi Bilioni 133,259,933,855.

Hasunga ametoa takwimu hizo tarehe 15 Disemba 2018 wakati akizungumza kwenye mkutano wa wabanguaji uliofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.

Amesema kuwa katika Mkoa wa Mtwara wananchi ambao wamekwishalipwa ni 77,055 huku jumla ya fedha iliyolipwa ni Bilioni 80,098,982,060.

Katika mkoa wa Lindi tayari wakulima 41,564 wamekwishalipwa kiasi cha Bilioni 42,502,635,227 huku katika mkoa wa Ruvuma wakulima 11,463 wamekwishalipwa kiasi cha Bilioni 10,557,222,943.

Aidha, Mhe Hasunga amesema kuwa katika mkoa wa Pwani Milioni 101,091,960 zimekwishalipwa kwa wakulima 81.

Alisisitiza kuwa vyama vilivyohakikiwa ni 461 na vilivyolipwa ni 451, ambapo jumla ya Kilo 40,381,798.

Bongo Movie sasa usoni mwako, Tazama hapa
Njia 6 Rahisi za Kuwa Imara Wiki Yako ya Kwanza Kazini