Muamuzi Cagatay Sahan pamoja na wasaidizi wake waliochezesha mchezo wa ligi ya nchini Ugiriki kati ya Trabzonspor dhidi ya Gaziantepspor, walijiokuta matatani baada ya kufungiwa ndani ya chumba cha kubadilishia nguo.

Maafisa wa klabu ya Trabzonspor wanadaiwa waliamuru waamuzi wafungiwe kwenye chumba cha kubadilishia kwa saa kadhaa, kufutia mkasa wa kuwanyima mkwaju wa penati dhidi ya mahasimu wao wa jadi Gaziantepspor.

Inadaiwa kuwa maafisa wa klabu ya Trabzonspor walihisi Sahan, aliwanyima nafasi ya kuibuka na ushindi katika mchezo huo, alipoamuru mchezo uendelee ilihali mchezaji wao aliangushwa kwenye eneo la hatari dakika za lala salama.

Mbali na maamuzi ya kufungiwa chumbani, pia muamuzi huyo alionyesha kuwakasirisha mashabiki wa Trabzonspor ambao walijaribu kuvuruga hali ya utulivu uwanjani hapo, lakini maafisa wa usalama walifanikiwa kuzima tukio hilo.

Rais wa klabu ya Trabzonspor, Ibrahim Haciosmanoglu anadaiwa kuhusika na hatua za kufungiwa kwa waamuzi hao, baada ya kutoa amri ya jambo hilo kufanyika.

Haciosmanoglu inadaiwa aliruhusu waamuzi hao watolewe kwenye chumba walichokua wamefungiwa, baada ya kuzungumza na rais wa nchi hiyo, Recep Tayyip Erdogan.

Shirikisho la soka nchini Uturuki limeanzisha uchunguzi dhidi ya tukio hilo na ikibainika kulikua na hatua zilizokiukwa, hatua kali za kinidhamu zitaelekezwa kwa wahusika.

Dkt. Magufuli, Samia Wakabidhiwa Vyeti Vya Ushindi
Mchezaji Wa Chelsea Asakwa Na Polisi