Ikiwa ni siku ambayo Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha inatarajia kutoa hukumu ya kesi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili wanaokabiliwa na tuhuma za unyang’anyi wa kutumia silaha, idadi kubwa ya watu wamefika mahakamani hapo.

Idadi hiyo imeonekana mapema huku watuhumiwa wakifikishwa mahakamani hapo majira ya saa tatu asubuhi, hali iliyoashiria kuwa leo itakuwa tamati ya shauri hilo katika mahakama hiyo.

Sabaya alifika mahakaani hapo akisindikizwa na askari wa Jeshi la Magereza, huku akionekana kutabasamu zaidi.

Hakimu Mkazi Mfawithi wa Mahakama hiyo, Amalia Mushi ndiye aliyepanga tarehe ya leo kama siku ambayo hukumu ya kesi hiyo itatolewa, baada ya kuahirishwa Oktoba 1.

Sabaya na wenzake wawili wamefikia hatua hiyo baada ya upande wa Jamhuri kuwasilisha vielelezo nane na mashahidi 11 dhidi yao.

Sabaya na wenzake wawili walikamatwa Mei 27, 2021 jijini Dar es Salaam na kufikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Juni 4, 2021.

Serikali ya aahidi kutatua migogoro ya ardhi
Polisi amuua mtoto wa miaka 5 kwa risasi, wananchi waingia mtaani