Kiungo wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Mudhathir Yahya, bado anashikilia Rekodi ya kuwa mchezaji mzawa pekee aliyefunga Hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Hadi sasa Young Africans imeshafunga mabao manane, mabao saba yakifungwa na wachezaji wa Kigeni, huku Klabu hiyo ya Wananchi ikitinga Hatua ya Robo Fainali.

Mudhathir alipachika bao hilo kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, wakati wa mchezo wa mzunguuko wapili wa Kundi D dhidi TP Mazembe ya DR Congo iliyokubali kipigo cha 3-1, akitumia pasi ya Kennedy Musonda raia wa Zambia.

Rekodi hiyo ya Mudathir inaihusisha hadi Simba SC inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Barani Afrika ambayo imeshuhudia mabao yake katika michuano hiyo yakipachikwa na wachezaji wa kigeni

Hadi sasa Kinara wa upachikaji mabao katika michuano ya Kimataifa upande wa Young Africans ni Fiston Mayele (DR Congo) mwenye mabao matatu, Mzambia Kennedy Musonda (2), Jesus Moloko (1) na Tuisila Kisinda (1) woteraia raia wa DR Congo.

Upande wa Simba SC ambayo imetinga Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, mabao yote yamefungwa na wageni ambapo kinara ni Clatous Chama mwenye mabao manne, huyo ni raia wa Zambia, Hennock Inonga wa DR Congo (1), Jean Baleke kutoka DR Congo (2) na Sadio Kanoute raia wa Mali (2).

Kagera: Watumishi wa Afya, Wananchi wawekwa karantini
Wachezaji Azam FC wachimbwa mkwara mzito