Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuberi ametangaza kufunguliwa rasmi kwa madrasa zilizofungwa kutokana na mlipuko wa virusi vya Coorna nchini.

Amesema madrasa zote zilizofungwa zifunguliwe na kuanza kutoa huduma kama ilivyo kuwa awali, lakini kwa kuzingatia maelekezo ya wataalam wa afya.

“Madrasa zitakazorudi na kuanza kutoa huduma ni zile zenye wanafunzi ambao umri wao kidogo ni mkubwa, wale wadogo kabisa zitaendelea kufungwa” Amefafanua, Mufti Zuberi.

Kadhalika, amesisitiza madrasa zitakazofunguliwa kuanza kazi zinatakiwa kuchukua tahadhari zote ambazo zinaelekezwa na Wizara ya Afya.

OSHA watakiwa kuongeza nguvu, usimamizi sheria ya Usalama na Afya mahali pa kazi
Taharuki: Wimbi la pili maambukizi ya Corona China laibuka