Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amemuagiza Kamishna Mkuu wa Jeshi la Polisi la nchi hiyo kuwakamata wachezaji wote wa timu ya nchi hiyo walioenda nchini Brazil kushiriki mashindano ya Olympic bila kuambulia kitu.

Zimbabwe ilituma timu ya wachezaji 31 kwenye mashindano hayo lakini ni moja kati ya nchi ambazo hazikuambulia kitu.

Mugabe asema kuwa timu hiyo inapaswa kukamatwa kwa sababu imetumia pesa nyingi ya nchi huku akiifananisha na panya.

“Tumepoteza fdha za nchi kwa ajili ya hawa panya ambao tunawaita wanamichezo,” alisema Mugabe.

“Kama hatuko tayari kujotoa sadaka tukashinda hata shaba kama majirani zetu Botswana walivyofanya, sasa kwanini mlienda kupoteza pesa zetu?” alihoji.

“Kama tunataka watu waende Brazil tu kwa ajili ya kuimba wimbo wetu wa taifa na kupeperusha bendera, tungewatuma kati ya wasichana wetu wazuri na vijana watanashati kutoka Chuo Kikuu cha Zimbabwe kutuwakilisha,” anakaririwa.

Rais huyo mkongwe zaidi barani Afrika alisisitiza kuwa pesa zilizotumika kuwekeza kwenye timu hiyo ya taifa zingeweza kutumika kujenga shule na mambo mengine ya kimaendeleo.

Mkuu wa Idara ya Ardhi apewa siku mbili kutatua matatizo ya ardhi, Rukwa
Lowassa: Mkutano wa CCM Dodoma ulikuwa Mkutano wangu