Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amepitishwa na chama chake cha Zanu- PF kuwa mgombea urais katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo utakaofanyika mwaka 2018.

Wajumbe wa Zanu-FP walifikia uamuzi huo wa kumpa nafasi nyingine Mugabe mwenye umri wa miaka 92 kupitia mkutano wao uliofanyika katika mji wa kusini mashariki wa Masvingo.

Mugabe amelitawala taifa hilo tangu lilipopata uhuru mwaka 1980 lakini bado chama chake kinaonesha kuwa na imani naye huku kikieleza kuwa anafaa kuwa rais kwa maisha yake yote.

Chama hicho kimefikia uamuzi huo wakati ambapo kumekuwa na maandamano ya kupinga uongozi wa Mugabe kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni kupinga anguko la kiuchumi na hali mbaya ya maisha.

 

Majaliwa aagiza kaburi la Faru John Lifukuliwe
Video Mpya: Belle 9 Feat. G Nako – Give It to Me