Mshambuliaji wa Simba, raia wa DR Congo Chriss Mugalu, amerejea kuwavaa Yanga hii ni baada ya kukosa mechi mbili zilizopita kutokana na kuwa na maumivu ya msuli.

Mugalu ambaye mpaka sasa ana mabao 10 kwenye msimamo wa wafungaji bora Ligi Kuu Bara, aliumia mguu kwenye mchezo dhidi ya Polisi Tanzania ulioisha kwa Simba kushinda bao 1-0.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Bara ulichezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza na bao la ushindi lilifungwa na kiungo Luis Miqiussone aliyepachika bao hilo kwa pigo huru.

Daktari Mkuu wa Simba, Yassin Gembe amesema kuwa: “Hali ya Mugalu ipo vizuri kwa sasa na ameanza mazoezi na wenzake, yupo katika hali nzuri na ni chaguzi ya kocha kutaka kumtumia.

“Kwa sasa hatuna majeruhi hata mmoja wachezaji wote wapo sawa kuelekea mchezo dhidi ya Yanga.”

Kesho Jumamosi (Julia 3), Simba inatarajiwa kumenyana na Yanga kwenye mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Varane aitoa udenda Man Utd
Lissu aeleza siku atakayorudi Tanzania, atakachofanya