Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, Crispin Mugalu Mutshimba amefunguka kwa furaha kuhusu mazingira ya ushindani wa Ligi Kuu Tanzania Bara, msimu huu 2020-21.

Mugalu ambaye alisajiliwa Simba SC mwanzoni mwa msimu huu akitokea Lusaka Dynamos FC ya Zambia, amesema amefurahishwa sana na mazingira ya ushindani ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara, hasa baada ya kufanya vizuri kwa kuifungia mabao klabu yake.

Amesema ni vigumu sana kwa mchezaji yoyote kuzoea mazingira ya Ligi mpya anayocheza tena kwa msimu wake wa kwanza, lakini kwake imekua tofauti sana, hivyo hana budi kumshukuru Mungu na wadau wa Simba SC ambao wamekua wakimuonesha ushirikiano mkubwa.

“Ni Msimu wangu wa kwanza kucheza Ligi ya Tanzania, lakini ninafurahi kuona nimefanya vizuri kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu, ninachotamani hivi sasa ni kuwa Mfungaji Bora, baada ya timu yangu kutwaa ubingwa wa nne mfululizo.” amesema Mugalu

Hadi sasa Mugalu ameifungia Simba SC mabao 13, akitanguliwa na Mshambuliaji wa Azam FC Prince Dube mwenye mabao 14, huku Bocco akiendelea kuwa kinara katika orodha ya wafungaji Bora hadi sasa.

Miss Tanzania avuliwa uwakilishi miss world
CECAFA yasogeza mbele michuano ya kufuzu