Klabu ya Azam FC,  imethibitisha kuwa kwenye hatua za mwisho kumsajiki kiungo kutoka Kenya na klabu ya Gor Mahia Kenneth Muguna.

Mkuu wa Idara ya Habari ya Azam FC,  Thabit Zakaria *Zaka Zakazi* amesema dili la mchezaji huyo lipo katika hatua nzuri na ni vitu vichache vimebaki ili kukamilika.

“Kilichobaki kabla ya Kenneth Muguna kujiunga na klabu yetu ya Azam ni barua  ya kumruhusu  (Release letter) kutoka klabu ya Gor Mahia na malipo ya ambayo tunatakiwa kulipa CAF.”

“Tupo katika hatua za mwisho kulipa hizo pesa, kila kitu kitakaa  sawa, Muguna  atapokea kiasi Kilichobaki pindi tu atakapo wasili klabuni” amesema Zaka Zakazi.

Kenneth Muguna alikua anahusishwa na mpango wa kujiunga Young Africans, lakini taarifa za kuibukia Azam FC zinazima rasmi mpango wa klabu hiyo kongwe katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Fiston afungasha na kuondoka kambini
Kajala afuta tatto ya herufi 'H'