Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Othman Kiloloma ameeleza kusikitishwa na kitendo cha waandishi wa habari kupiga picha za wagonjwa na kuzionesha kwenye vyombo vya habari wakati Rais John Magufuli alipofanya ziara ya ghafla katika hospitali hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa, Othman Kiloloma

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa, Othman Kiloloma

Mkurugenzi huyo Mtendaji ameeleza kuwa kitendo hicho ni kinyume cha maadili ya uandishi wa habari na maadili ya udaktari.

“Yule mgonjwa amelala pale hana concept kwahiyo kitendo chake cha kuwa mgonjwa sio ruhusa kwa mwandishi wa habari kupiga picha na kuzirusha zikiwa vile. Hata zikiwa edited hatakiwi kuoneshwa pale, anaweza akawa baba yako, anaweza akawa shangazi yangu. Na hawa ni wagonjwa, kuna wakati mwingine wanaweza wakawa wamekaa vibaya kwahiyo kurusha picha katika hali walizokuwa nazo hiyo sio sahihi,” alisema.

Aliwataka waandishi wa habari kutotumia misafara ya viongozi wakubwa kupiga picha za aina hiyo kwakuwa wanajua hawawezi kudhibitiwa na uongozi wa hospitali hiyo wakati huo.

“Hili sisi kama uongozi wa Taasisi limetufadhaisha, nadhani katika maadili ya uandishi wa habari ni muhimu kuangalia ili kujenga utu na staha za wagonjwa wetu. Sisi ni wazima leo, kesho tutakuwa wagonjwa

 

 

 

Wa8 Wakamatwa Kwa Uharibu Wa Uwanja Wa Arsenal
Mavuno ya Pamba Yaongezeka, Wakulima Wasubiri Viwanda Vya Magufuli