Leo Juni 18, 2018 Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Taifa, Freeman Mbowe amelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kudondoka ghafla alfajiri akiwa nyumbani kwake.

Hayo yameelezwa leo mahakamani na wakili wake, Jeremiah Mtobesya pindi akiiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkuu Wilbard Mashauri.

Hata hivyo Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Aminiel Aligaesha amethibitisha kuwa mapema leo hii wamempokea Mbowe alipopigiwa simu na MCL Digital.

”Ni kweli tumempokea Mbowe leo asubuhi”, amesema Aligaesha.

Pia taarifa hizo zimethibitishwa na Mkurugenzi wa Itifaki na Mawasiliano Chadema, John Mrema.

Aidha Mbowe ambaye ni mshatakiwa namba 1 katika kesi namba 112 ya 2018 alitakiwa kufika mahakamani siku hii ya leo kusikiliza mashtaka yanayomkabili.

 

Haya ndiyo madhara ya ulaji ndizi kupita kiasi
Aliyemuua mhadhiri UDOM ashikiliwa na polisi

Comments

comments