Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imewapatia mafunzo elekezi watumishi wake wapya ili kuhakikisha watumishi hao wanafanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia maadili ya taaluma zao na maadili ya utumishi wa Umma.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Prof. Lawrence Museru ambapo amewasisitiza waajiriwa wapya kuwajibika na kutoa huduma inayostahili na kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wateja.

 “Jukumu la hospitali ni kutoa huduma bora na kwa upendo na si kuleta matatizo hivyo kila mtu atekeleze wajibu wake kama inavyotakiwa, wagonjwa wapewe tiba inayostahili na atakayeshindwa kutimiza majukumu yake atawajibishwa,’’ amesema Prof. Museru.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utumishi, Makwaia Makani amesema kuwa mafunzo hayo yana lenga kuwaelekeza waajiriwa wapya masuala ya utumishi wa Umma, miiko na taraibu zake.

Naye mtoa mada kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania –TACAIDS- Dkt. Hafidh Ameir amesema waajiri wana wajibu wa kuhakikisha watumishi wao wanapata taarifa za Ugonjwa wa Ukimwi pamoja na magonjwa yasiyoambukiza na kwamba suala hilo liwe ajenda ya kudumu katika taasisi zao.

Serikali yatangaza mnada wa madini ya Tanzanite
Magufuli awatahadharisha mabinti watembea utupu