Karibu Dunia nzima inazungumza juu ya tukio la kusikitisha lililofanywa kwa bahati mbaya na Muigizaji maarufu kutoka nchini Marekani, Alec Baldwin kumuua kwa kumpiga risasi Bi Halyana Huychins wakiwa katika eneo la kurekodia Filamu (On Set)

Baada ya ukimya kwa masaa kadhaa ya kutokea kwa tukio hilo, kwa mara ya kwanza Alec Baldwin ameutumia ukurasa wake wa mtandao wa twitter kuandika maneno yenye kudhihirisha kiwango cha huzuni aliyonayo baada ya kumuua kwa kumpiga risasi mshirika wake katika kazi Halyna Hutchins.

“Hakuna maneno ya kuelezea mshtuko na huzuni yangu juu ya ajali mbaya ambayo ilichukua uhai wa Halyna Hutchins, mke, mama na mwenzetu aliyevutia sana. Ninashirikiana kikamilifu na uchunguzi wa polisi kushughulikia  jinsi mkasa huu ulivyotokea” ameandika Baldwin.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Oktoba 23, 2021
Muigizaji amuua mwenzie kwa risasi wakiwa Location