Ajali haina kinga,

Hii ni miongoni mwa misemo maarufu wenye kuishi katika maisha ya binaadam kwenye kila sekunde ya uhai.

Msemo huu umelazimika kuzidhiti hasira na maumivu ya wahanga wa tukio la mauaji ya  muongozaji wa picha mjongea (Director Of Photography) Halyna Hutchins aliyeuawa kwa kupigwa risasi bila kukusudia na Muigizaji maarufu wa nchini Marekani Alec Baldwin wakiwa katika eneo la kurekodia filamu (On Set) huko New Mexico Nchini Marekani.

Baldwin ameripotiwa kumuua bila kukusudia Halyna Hutchins na kumjeruhi vibaya Joel Sauza ambae ni Director wa filamu ‘Rust’ kwa kutumia bunduki waliyokuwa wakiitumia katika filamu hiyo ikiaminika kuwa ni bunduki ya bandia.

Hadi sasa Polisi wanaendelea na Uchunguzi zaidi na kwa mujibu wa ripoti ni kuwa hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusu tukio hilo.

Siku mbili kabla ya kifo chake,  Halyna Hutchins mwenye umri wa miaka 42, aliandika juu ya furaha ya kufanya kazi kwenye sinema ya Rust katika jangwa la New Mexico. “Moja ya faida ya kufanya kazi (shooting) magharibi ni kwamba utapanda farasi siku yako ya kupumzika,” aliandika kwenye Instagram, maneno yaliyo ambata na video ya selfie, ikimuonyesha kiwa juu ya farasi na kundi la watu kadhaa.

Muigizaji Alec Baldwin aongea baada ya kuua
Tanzania na Burundi kuimarisha mipaka