Muigizaji maarufu wa Afrika kusini ameripotiwa kupigwa risasi mbili na watu wasiojulikana walivamia nyumbani kwake jana usiku wa manane, jijini Johannesburg.

Taarifa zilizothibitishwa na jeshi la polisi nchini humo zimeeleza kuwa jina la muigizaji huyo bado limehifadhiwa kwa sababu maalum lakini walieleza kuwa ni muigizaji wa kike.

Msemaji wa huduma za dharura, Chris Botha amesema kuwa muigizaji huyo alijeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu. Alisema yuko katika hali mbaya ingawa anazidi kuimarika hospitalini hapo.

Vyombo vya usalama vimeeleza kuwa vitatoa taarifa kamili ikiwa ni pamoja na kuweka wazi jina la muigizaji huyo.

FIFA Wainyooshea Kidole Mexico
Mfalme wa Saudi Arabia amchagua mwanae kumrithi, amvua binamu yake