Muigizaji wa filamu maarufu za ‘Star Wars’, Andrew Jack amefariki dunia baada ya kushambuliwa na virusi vya corona (covid-19), juzi, Machi 31, 2020 akiwa na umri wa miaka 76.

Kwa mujibu wa wakala wake, Jill McCullough muigizaji huyo ambaye pia alikuwa mkufunzi wa mazungumzo kwenye ‘Star Wars’, alipoteza maisha akiwa anapatiwa matibabu hospitalini huko Surrey.

“Andrew alikuwa akiishi kwenye moja kati ya nyumba zake za muda mrefu, alikuwa anajitegemea lakini alikuwa ana mahaba tele kwa mkewe,” alisema McCullough.

Jack alishiriki katika ‘Star Wars: Episode VIII – The Last Jedi’, akiwa kama Jenerali Emmat, na pia kwenye ‘Solo: A Star Wars Story’ na ‘Star Wars: Episode VII – The Awakens.’

Mkewe Gabrielle Rogers ambaye amewekwa Karantini nchini Australia, ameweka ujumbe kwenye mitandao ya kijamii, “Andrew Jack alikuwa anapatiwa matibabu baada ya kubainika kuwa ana virusi vya corona siku mbili zilizopita. Hakuwa na maumivu, na alilala kwa amani akijua familia yake yote iko pamoja naye.”

Miraji Athumani: Sasa nipo sawa
Kizimbani kwa kuzalisha na kupelekea kifo cha Mama na vichanga