Polisi nchini Cyprus wamesema kuwa wanamshikilia raia mmoja wa Israel anayetuhumiwa kufanya biashara ya viungo vya binadamu.

Moshe Harel amehusishwa kufanya biashara ya figo kwa matajiri wa Israel kwa takribani miaka kumi, ambapo amehusishwa kuchukua figo za raia wa Kosovo pamoja na Uturuki na nchi nyingine kadhaa ambao mpaka sasa hajawalipwa chochote.

Aidha, Msemaji wa polisi nchini Cyprus amesema kuwa mtu huyo alikamatwa uwanja wa ndege wa Larnaca mwezi Desemba mwaka jana.

Hata hivyo, Harel anatarajiwa kufikishwa mahakamani siku ya Jumanne kujibu mashtaka yanayomkabili.

Mapigano makali yazuka nchini Misri
Mawaziri wawili wakamatwa kwa rushwa