Kiungo kutoka DR Congo Mukoko Tonombe amewaomba radhi mashabiki na wanachama wa klabu ya Young Africans kufuatia adhabu ya kadi nyekudu aliyoipata jana Jumapili (Julai 25), wakati wa mchezo wa Fainali Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba SC.

Mukoko alioneshwa kadi nyekundu dakika chache kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika Uwanja wa Lake Tanganyika, kufuatia kumpiga kiwiko nahodha na Mshambuliaji wa Mabingwa wa Tanzania Bara Simba SC John Raphael Bocco.

Mukoko amewaomba radhi mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kongwe katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na ujumbe wake umewekwa kwenye ukurasa wa instagram wa Young Africans.

Mukoko amesema: Nachukua fursa hii kuwaomba radhi mashabiki, viongozi na benchi la ufundi kwa kilichotokea katika mchezo wa Fainali wa Yanga Vs Simba SC.

Kwamba sijakusudia kupewa kadi nyekundu ambayo labla ndio ilikua sababu ya kupoteza mchezo huo. Naipenda sana timu yangu Yanga.


Daima Mbele Nyuma Mwiko.
Mukoko Tonombe.


Katika mchezo huo Young Africans walikubali kufungwa bao 1-0, na kupoteza bahati ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ uliokwenda kwa watani zao Simba SC kwa mara ya pili mfululizo.

Bao la ushindi kwa Simba SC lilifungwa na kiungo kutoka nchini Uganda, Thadeo Lwanga dakika ya 80 kwa kichwa akimalizia mpira wa kona uliopigwa na kiungo wa kimataifa kutoka Msumbiji, Jose Luis Miquissone.

Mtoto afariki kwa kutumbukia kisimani
Wewe mtanzania wala usiikimbie nchi yako - Waziri Nchemba