Wananchi wanaoishi katika visiwa 39 vilivyoko katika Ziwa Victoria upande wa wilaya ya Muleba, mkoani Kagera wameanza kunufaika na huduma za afya zitolewazo na meli tiba ya MV.JUBILEE HOPE, baada ya halmashauri ya wilaya hiyo kuzindua awamu ya pili ya utoaji wa huduma hizo.

MKUU wa wilaya ya Muleba Mkoani Kagera Toba Nguvilla amezindua huduma ya Meli ya Matibabu (Medical Ship) Mv Jubilee Hope kwa wakazi wa Visiwani hivyo ili kuweza kuondokana na changamoto ambazo walizokuwa wanakumbana nazo wananchi awali.

Mkuu wa Wilaya ya Muleba katika uzinduzi wa Meli hiyo

Uzinduzi wa meli hiyo ya matibabu ulihudhuriwa pia na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muleba Elias Mahwago
Kayandabila na viongozi wengine ambao wamefurahia uwepo wa huduma hiyo muhimu.

Mkurugenzi wa Wilaya ya Muleba akitia sahihi katika kitabu cha wageni ndani ya meli hiyo.

Hatua hiyo inatajwa kwamba itakuwa mkombozi kwa wananchi wa maeneo hayo yenye Kata 43 huku kata 5 za Mazinga, Ikuza, Bumbile, Kerebe na Goziba zikiwa ndani ya Ziwa Victoria na kwa ujumla wake inakadiriwa kuwa na wakazi takribani 68,000 kwa majibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.

Meli hiyo iliyotolewa na Shirika la Vine Trust lililopo nchini Uingereza inasimamiwa na kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Geita kwa kushirikiana na mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) ilianza kutoa huduma mwaka 2015 na mkataba uliisha 2020.

Kwa mujibu wa katibu mkuu wa kanisa la Africa Inland church Dayosisi ya Geita, Samweli Limbe amesema mkataba wa meli hiyo kuendelea kutoa huduma hakuweza kusaini kwa haraka kutokana na kuibuka kwa ugonjwa wa Corona, ila kwa sasa tayari umesainiwa ambapo meli hiyo itatoa huduma kwa muda wa miaka mitano mingine.

Kwa kutambua umuhimu na maelekezo ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2020 Halmashauri ya Wilaya ya Muleba imeamua kusajili Meli hiyo kama
Kituo cha Afya kwa upande wa ziwani ambapo Tsh. 119 milioni zimelipwa MSD ili kupata uhakika wa madawa kwa wananchi.

Radi yaua watu zaidi ya watano.
Shehena ya parachichi yaelekea India